• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa UM aonya kuwa vijana wanakabiliwa na ukosefu wa elimu

    (GMT+08:00) 2019-08-12 17:53:42

    Ikiwa leo dunia inaadhimisha siku ya vijana, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ameonya kuwa vijana wengi wanakabiliwa na ukosefu wa elimu, na kukosoa shule kwa kutowafundisha vijana ujuzi mbalimbali unaohitajika kwenye mageuzi ya teknolojia.

    Kauli mbiu ya siku ya vijana mwaka huu ni "Geuza elimu", ambayo lengo lake ni kuhimiza juhudi ili kuifanya elimu iwe inafaa zaidi, iwe na usawa na iwe shirikishi kwa vijana wote, ikiwemo juhudi za vijana wenyewe.

    Bw. Guterres ameongeza kuwa shule zinatakiwa kuwafundisha ujuzi wa maendeleo endelevu na mabadiliko ya hali ya hewa, na kueneza maoni ya usawa wa jinsia, kulinda haki za binadamu na utamaduni wa amani.

    Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, zaidi ya nusu ya watoto au vijana walio na umri kati ya miaka 6 na 14 hawajui kusoma na kuhesabu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako