• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Lionesses na Simbas wasalia katika nafasi zao viwango vya raga

  (GMT+08:00) 2019-08-13 08:05:39
  Timu za raga za Kenya za wachezaji 15 kila upande za Lionesses (wanawake) na Simbas (wanaume) zimesalia katika nafasi za 28 na 32 kwenye viwango bora vya dunia vilivyotangazwa mwishoni mwa wiki. Lionesses ililipua Makis ya Madagascar 35-5 Agosti 9 katika mechi ya ufunguzi ya mchujo wa kuingia Kombe la Dunia mwaka 2021 inayoendelea jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini. Warembo wa kocha Felix Oloo watarejea uwanjani kuvaana na mahasimu wa jadi Uganda hii leo. Afrika Kusini inasalia nambari moja barani Afrika na inashika nafasi ya 11 duniani. Inafuatiwa na Kenya (28 duniani), Zambia (35), Namibia (39), Madagascar (41), Zimbabwe (42) na Uganda (45).
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako