• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yailaani Marekani kwa kuifanya kanda ya Ghuba iwe ya kijeshi

    (GMT+08:00) 2019-08-13 09:04:44

    Waziri wa mambo ya nje wa Iran Mohammad Javad Zarif jana amesema, kitendo cha Marekani kuziuzia silaha nchi za kanda ya Ghuba kumeifanya kanda hiyo "iwe bomu ambalo liko tayari kulipuka".

    Zarif ametolea mfano matumizi ya nchi za Falme za Kiarabu (UAE) na Saudi Arabia kwenye manunuzi ya silaha, akisema Marekani iliuza silaha zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 50 kwa kanda ya Ghuba mwaka jana.

    Zarif amesema matishio ya kanda hiyo yanatokana na Marekani na washirika wake ambao wanamwaga silaha kwenye kanda hiyo, huku akiituhumu Marekani kutaka kuunda muungano wa kijeshi baharini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako