• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mashirika ya ndege ya Afrika yaendelea kuimarika

  (GMT+08:00) 2019-08-13 19:14:02
  Shirika la kimataifa la uchukuzi wa anga IATA limesema kuwa mashirika ya ndege ya Afrika yameendelea kuimarika kwa kuongeza idadi ya ndege na abiria.

  Ripoti ya IATA ya 2018 inaonyesha kuwa mashirkka ya ndege ya Afrika yalisafirisha abiria milioni 92 kati ya bilioni 4.4 kote duniani.

  Shirika hilo limesema idadi hiyo inawakilisha ukuaji wa asilimia 5.5.

  Eneo la Asia-Pacific ndio lililoandikisha idadi kubwa ya wasafiri kwa kufikia bilioni 1.6 ikiwa ni asilimia 37.

  Eneo hilo lilikuwa na ongezeko la 9.2 huku nayo Ulaya na Amerika Kaskazini yakiwa na ukuaji wa asilimia 26 na 22.

  IATA imesema ushindani umesaidia kuanza kwa mashirika yenye bei nafuuu ya usafiri.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako