• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Match Maker yawekeza sekta ya mifugo

  (GMT+08:00) 2019-08-13 19:14:40
  Mchakato wa kuwaanda Watanzania kuzalisha kwa wingi malighafi ya viwandani wakati Tanzania ikielekea katika uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, umeanza kuwavutia wawekezaji wa sekta ya mifugo na mazao yake kuwekeza kulingana na mahitaji ya soko.

  Kampuni ya Match Maker Tanzania ambayo inafanya kazi kwa karibu na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV), linaloendesha mradi wa faida maziwa kwa wafugaji wa wilaya za Hai na Siha, mkoani Kilimanjaro, imeeleza nia yake ya kuendelea kuwawezesha wafugaji wa ng'ombe wa maziwa kufuga kulingana na mahitaji ya masoko la maziwa ndani na nje ya nchi.

  Mkurugenzi wa Kampuni ya Match Maker, Peniel Uliwa, ameeleza kuwa mpango wa huo una lenga kuchochea ajira, ustawi endelevu wa jamii na kufungua fursa za upatikanaji wa malighafi ya viwandani kupitia sekta ya mifugo na hasa ufugaji wa kisasa wa ng'ombe wa maziwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako