• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Limuru Tea yapata hasara ya Kampuni ya shilingi milioni 18

  (GMT+08:00) 2019-08-13 19:15:03
  Kampuni ya Chai ya Limuru imepata hasara ya shilingi milioni 18 katika kipindi cha miezi 6 ya kwanza ya 2019.

  Kampuni hiyo imesema hasara hiyo ni mara 7 ya ile iliopata kipindi sawa na hicho mwaka jana.

  Mauzo yake ya hadi mwishoni mwa Juni yalifikia milioni 29 iliwa ni upungufu wa kutoka milioni 42 mwaka 2018.

  Mwenyekiti wa kampuni hiyo Richard Korir amesema kudorora kwa mapato kumechangiwa na kushuka kwa bei ya chai kwenye soko la kimataifa.

  Kampuni nyingine za chai pia zimetumbukia kwenye hasara huku ile ya Eaagads tayari ikitoa taarifa ya kuwa na uwezekano wa hasara.

  Sasini Tea ilipata hasara ya shilingi milioni 194 katika kipindi kilichokamilika machi 2019.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako