• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Safari za ndege zasitishwa Hongkong kutokana na maandamano haramu

  (GMT+08:00) 2019-08-14 08:31:23

  Mamlaka ya viwanja vya ndege katika mkoa wenye utawala maalum wa Hongkong, China imetangaza kusitisha huduma zote za safari za ndege baada ya uwanja huo kuzidiwa na waandamanaji.

  Mamlaka hiyo imewataka abiria waondoke kwenye uwanja huo haraka iwezekanavyo, na kutoa wito kwa watu mashuhuri kuepuka kwenda kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hongkong. Aidha, Kituo cha Dharura katika uwanja huo kimefunguliwa.

  Mamlaka hiyo imesema inadumisha mawasiliano ya karibu na mashirika ya ndege na wadau mbalimbali, na kutumai kuwa huduma za kawaida zitarejeshwa mapema iwezekanavyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako