Kwa upande wa timu ya wanawake ya mgongo ya Kenya, timu hiyo imepata alama moja muhimu dhidi ya Ghana japo kwa jasho katika mechi yake ya pili ya kina dada kwenye mchujo wa mpira wa magongo wa Afrika wa kufuzu kushiriki Olimpiki mwaka 2020, ambayo ilimalizika kwa sare ya 1-1 nchini Afrika Kusini katika mechi iliyochezwa jana. Rhoda Kuira aliifungia Kenya bao la mapema katika dakika ya saba kutokana na kona fupi. Hata hivyo, kutoka hapo warembo hao walishambuliwa hadi kipenga cha mwisho. Mashambulizi makali ya Ghana yalishuhudia ikisawazisha 1-1 kupitia kwa Mavis Berko kutokana na kona fupi. Wakenya waliponea mara kadhaa kuadhibiwa na Ghana kwa kupoteza mipira kwa urahisi. Matokeo haya yaliendeleza rekodi nzuri ya Kenya kutoshindwa na Ghana katika mechi za kufuzu kushiriki Olimpiki hadi mechi nne.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |