• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mawakala wa Ozil sasa kutua nchini Amerika kufanikisha uhamisho wake hadi DC United

  (GMT+08:00) 2019-08-14 08:53:21
  Vinara wa kikosi cha DC United nchini Amerika wamemtaka kiungo Mesut Ozil kukubali mshahara mdogo ili ajiunge na miamba hao wa Major League Soccer (MLS) wanaopania kulijaza pengo la Wayne Rooney. Ozil kwa sasa ndiye mchezaji wa pili baada ya Alexis Sanchez wa Manchester United anayepokea mshahara wa juu zaidi katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL). Nyota huyu wa zamani wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ujerumani kwa sasa hupokea Sh46 milioni kwa wiki. Kiini cha DC United kuyataka maarifa ya Ozil ni kujaza nafasi ya Rooney ambaye kwa sasa anajiandaa kuanza majukumu ya kuwa kocha na mchezaji wa Derby County mnamo Januari 2020.
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako