• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • UM yasema msaada wa kibinadamu kwa Aden, Yemen utaendelea kuwa kipaumbele licha ya kuongezeka kwa vurugu

  (GMT+08:00) 2019-08-14 09:30:48

  Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric amesema licha ya kuongezeka kwa vurugu mjini Aden, Yemen, Umoja huo utaendelea na shughuli za kusambaza msaada wa kibinadamu mjini humo na mikoa ya jirani. Kwa mujibu wa Mratibu Mkazi wa Masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, ripoti za awali zimesema kuwa watu 40 wameuawa na wengine 260 kujeruhiwa tangu tarehe 7, Agosti. Bw. Dujarric pia amesema Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa pande zote kudumisha makubaliano ya kusimamisha vita mjini Aden na kushiriki katika mazungumzo ili kutatua tofauti zao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako