• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watu watatu wahukumiwa kifo kwa kumuua mtu mwenye ulemavu wa ngozi nchini Malawi

  (GMT+08:00) 2019-08-14 18:58:24

  Mahakama kuu ya Malawi imewahukumu adhabu ya kifo wanaume wawili na mwanamke mmoja kwa kumuua mtu mmoja mwenye ulemavu wa ngozi.

  Watu hao watatu waliotambuliwa kama Douglas Mwale, Fontino Folosani na Sophie Jere wameshtakiwa kumwua mlemavu wa ngozi Priscott Pepuzani mwaka 2015, kwa kumkata mikono na miguu na kuuzika mwili wake kwenye bustani,

  Jaji Esmie Chombo wa mahakama iliyoko wilaya ya Mchinji mkoa wa Kati wa Malawi amesema, hukumu hiyo itasaidia kuwaonya na kuwazuia wengine kufanya uhalifu unaofanana, wakati mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi yakiendelea kuongezeka.

  Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchi hiyo, mauaji zaidi ya 25 ya walemavu wa ngozi yameanza kutokea tangu mwaka 2014, na kueneza uwoga katika jamii ya watu wenye ulemavu wa ngozi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako