• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri wa Afya wa Afrika Kusini azua wasiwasi juu ya mswada wa afya wenye utata

  (GMT+08:00) 2019-08-14 19:46:36

  Waziri wa Afya wa Afrika Kusini Zweli Mkhize leo ameibua wasiwasi juu ya mswada wa Bima ya Afya ya Taifa NHI ambao umekuwa ukitiliwa mashaka tangu kuwasilishwa kwake.

  Mkhize amesema ana uhakika kwamba mswada utakapopitishwa, utaleta manufaa kwa afya ya watu nchini. Mswada huo uliowasilishwa bungeni na Mkhize wiki iliyopita, unalenga kutoa kifurushi cha kina cha huduma za afya bure kwenye vituo vya afya vya umma na binafsi ikiwa ni sehemu ya juhudi za serikali kuwezesha utoaji sawa wa huduma bora za afya. Hata hivyo mswada huo ambao unaaminika kuwa utawanufaisha watu wengi wakiwemo wafungwa, wakimbizi, wakazi wa kudumu na watoto wa Afrika Kusini, umekuwa ukitiliwa mashaka na pande mbalimbali za siasa na vyombo mbalimbali wakisema hauna uhalisia, una gharama kubwa, na unaweza kuharibu sekta ya afya, hasa wakati nchi inapokabiliwa na mgogoro wa fedha.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako