• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watu watatu wamefariki na wengine wawili hawajulikani walipo kufuatia ajali ya boti huko Lagos Nigeria

  (GMT+08:00) 2019-08-14 19:46:58

  Watu watatu wamethibitishwa kufa na wengine wawili hawajulikani walipo kufuatia ajali ya boti iliyotokea mjini Lagos.

  Akiongea na wanahabari mkuu wa Mamlaka ya Majini ya Lagos Oluwadamilola Emmanuel amesema boti mbili za abiria zilizobeba jumla ya watu 18, ziligoganga uso kwa uso jana kwenye mkondo wa Irewe katika eneo la Ojo. Emmanuel amesema abiria 13 wameokolewa na wazamiaji huku operesheni ya utafutaji na uokozi ikiendelezwa na mashirika husika ya jimbo. Mtu mzima mmoja na mtoto wametambuliwa kuwa ni watu wasiojulikana walipo. Uchunguzi wa awali uliofanywa na mamlaka unaonesha kuwa tukio hilo lilitokana na kitendo cha uzembe cha kuendesha kwa kasi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako