• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sintofahamu yatokea wakati timu ya wanariadha nchini Kenya ikielekea kwenye mashindano ya Afrika

    (GMT+08:00) 2019-08-15 08:34:40
    Sintofahamu na mpangilio mbovu vimetokea wakati kundi la kwanza la timu ya taifa ya wanariadha ya Kenya inaondoka kuelekea Rabat, Morocco, kwa ajili ya mashindano ya 12 ya Michezo ya Afrika ambayo yanatarajiwa kuanza jumatatu ijayo. Jana, wanariadha 11 na maofisa watano waliondolewa kwenye timu ya Kenya kutokana na uhaba wa fedha. Kenya imekuwa ikipata medali nyingi katika michezo ya riadha, na timu hiyo ina wachezaji wa zamani ambao wamefanya vizuri katika mashindano makubwa ya kimataifa. Wakati huohuo, timu ya taifa ya mchezo wa Chess ya Kenya nayo imeondoka leo kuelekea Rabat, Morocco kushiriki mashindano hayo, ikiwa na lengo la kupata ushindi katika mchezo huo. Kutokana na uhaba wa fedha, timu hiyo itapeleka wachezaji wanne.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako