• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ulinzi Stars yaanza michezo ya wanajeshi ya Afrika Mashariki kwa kumiminia Burundi mabao 4-0

    (GMT+08:00) 2019-08-15 08:35:51
    Wenyeji Ulinzi Stars ya Kenya wameanza kampeni ya kutetea taji la soka kwenye michezo ya Majeshi ya Muungano wa Afrika Mashiriki (EAC) kwa kishindo baada ya kuichabanga Burundi 4-0 jumanne wiki hii katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani jijini Nairobi. Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Kenya (KPL) mwaka 2003, 2004, 2005 na 2010, walipata mabao hayo muhimu kutoka kwa washambuliaji Oscar Wamalwa (matatu) na Enosh Ochieng'. Wamalwa alitikisa nyavu za Burundi katika dakika ya saba na kuimarisha uongozi huo katika dakika ya 57. Mfungaji bora wa KPL msimu 2018-2019 Ochieng', ambaye aliingia kama mchezaji wa akiba katika kipindi cha pili, alifuma wavuni bao la tatu dakika ya 76 kabla ya Wamalwa kupata 'hat-trick' yake dakika mbili baadaye.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako