• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maskauti wa Galatasaray watua London kutafuta huduma za Wanyama

    (GMT+08:00) 2019-08-15 08:36:11
    Maskauti wa kikosi cha Galatasaray cha Uturuki wametua jijini London, Uingereza kuanzisha mazungumzo yatakayomshuhudia kiungo Victor Wanyama akiondoka kwenye timu Tottenham Hotspur. Kwa mujibu wa gazeti la Fanatik nchini Uturuki, ujumbe wa Galatasaray nchini Uingereza upo chini ya mkurugenzi wao wa soka Sukru Haznedar ambaye anatazamiwa kuwashawishi Tottenham kumwachilia nahodha huyu wa Harambee Stars kufikia Agosti 31, 2019. Mbali na Wanyama, Galatasaray wanapania pia kujinasia huduma za kiungo matata wa Chelsea, Tiemoue Bakayoko kabla ya muhula wa usajili miongoni mwa vikosi vya Ligi Kuu ya Uturuki kumalizika rasmi mwishoni mwa mwezi huu. Kinachosubiriwa kwa sasa na usimamizi wa Galatarasay ni ripoti ya Haznedar ambaye anadai kuwa, dalili zote zinaashiria kwamba Spurs watakuwa radhi kuagana na Wanyama aliyewahi kuhusishwa pia na klabu za Fenerbahce, West Ham United na Bournemouth.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako