Kulingana na data za Benki Kuu ya Rwanda ambazo zilitolewa jana,mauzo ya nje yaliongezeka kwa asilimia 7.5 na bidhaa ambazo Rwanda iliagiza kutoka nje ziliongezeka kwa asilimia 18,na kusababisha nakisi kubwa ya biashara.
Gavana wa Benki ya Rwanda John Rwangombwa alisema bidhaa ambazo kwa kawaida huuzwa sana nje kama vile madini,chai na kahawa hazikufanya vizuri lakini wamepata utendaji mzuri katika bidhaa ambazo sio kawaida kuuzwa nje haswa zile zilizoundwa Rwanda.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |