• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Faida ya nusu mwaka ya benki ya KCB yaongezeka kwa asilimia 5 hadi Sh12.7bn

    (GMT+08:00) 2019-08-15 18:25:22
    Faida ya Benki ya KCB katika miezi sita ya kwanza ya mwaka 2019 imefika Sh12.7 billion, asilimia tano zaidi ikilinganishwa na kipindi sawa na hicho mwaka jana.

    Matokeo hayo yalitolewa wakati ambapo kuna ongezeko la asilimia tano katika mapato ya riba yaliyofika Sh25.4 bilioni huku mapato yasiyofadhiliwa yakikua kwa asilimia 15 hadi Sh13.2 bilioni.

    Afisa Mkuu Mtendaji wa benki ya KCB Lawrence Kimathi jana alisema faida hiyo imetokana na kutokuwa na mikopo mingi isiyolipwa kama ilivyokuwa mwaka jana.

    Matokeo hayo yameiweka benki ya KCB mbele ya mshindani wake wa karibu benki ya Equity ambayo ilifunga kipindi hicho na faida ya Sh11.92 bilioni.

    Ukuaji wa KCB katika mapato ya riba umesukumwa na ukuaji wa asilimia 13.8 katika mikopo na kuongeza riba katika mikopo kwa wateja hadi Sh479 bilioni kutoka Sh421 bilioni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako