• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani kupandisha ngazi ya mikwaruzano ya kibiashara kati yake na China kuzidi kuharibu biashara ya rejareja ya nchi hiyo

    (GMT+08:00) 2019-08-15 19:13:26

    Hivi karibuni Ikulu ya Marekani imeendelea kupandisha ngazi ya mikwaruzano ya biashara kati ya China na Marekani. Vyombo vya habari vya Marekani vinasema, hatua husika za Marekani zitazidi kuharibu biashara ya rejareja ya nchi hiyo.

    Shirika la Utangazaji la CBS la Marekani limesema, tishio jipya la Marekani la kuongeza ushuru dhidi ya bidhaa za China limesababisha kampuni za biashara ya rejareja za nchi hiyo kufunga maduka mengi zaidi na kuwafukuza wafanyakazi wengi zaidi kazini.

    Uchunguzi husika unaonesha kuwa, tangu mwaka huu uanze idadi ya maduka yaliyofungwa nchini Marekani imezidi ya mwaka mzima wa 2018, ambayo yalisababisha kiwango cha juu zaidi cha wafanyakazi waliofukuzwa katika miaka 10 iliyopita. Hadi kufikia mwezi Julai, sekta ya biashara ya rejareja ya Marekani imepunguza nafasi elfu 43 za ajira na kuongezeka kwa asilimia 40 ikilinganishwa na mwaka jana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako