• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa China na Brazil wapongezana kwa kuadhimisha miaka 45 ya uhusiano wa kibalozi

    (GMT+08:00) 2019-08-15 19:26:13

    Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Brazil Jair Messias Bolsonaro wamepongezana kupitia simu kwa kusherehekea maadhimisho ya miaka 45 tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kibalozi.

    Rais Xi amesema, China na Brazil zote ni nchi kubwa zinazoendelea na ni soko muhimu linalojitokeza. Katika miaka 45 iliyopita, uhusiano kati ya nchi hizo mbili umeimarishwa siku hadi siku, na ushirikiano wao umepata maendeleo makubwa katika sekta mbalimbali, ambayo yanaleta maslahi halisi kwa watu wa nchi hizo mbili na kuwa mfano wa kuigwa wa mshikamano na maendeleo ya pamoja kati ya nchi zinazoendelea.

    Naye rais Bolsonaro amesema, tangu Brazil na China zianzishe uhusiano wa kibalozi, nchi hizo mbili zimeshika lengo la maendeleo ya pamoja, na kufanya ushirikiano katika sekta mbalimbali na kuona fahari kwamba mifumo wa ushirikiano inaendelea kuboreshwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako