• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UM walaani mashambulizi dhidi ya vifaa na wafanyakazi wa afya Tripoli

    (GMT+08:00) 2019-08-16 09:12:48

    Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya Ghassan Salame amelaumu mashambulizi dhidi ya wafanyakazi wa afya na vifaa vya matibabu yaliyotokea mji wa Tripoli, ambao umeshuhudia mapigano ya kisilaha kati ya serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa na jeshi lenye makao makuu mashariki mwa nchi hiyo. Tume ya Msaada ya Umoja wa Mataifa nchini Libya UNSMIL imesema baada ya mapigano kuibuka mjini Tripoli mapema Aprili, mashambulizi zaidi ya 37 yamerekodiwa dhidi ya wafanyakazi na vifaa vya matibabu zikiwemo hospitali na magari ya wagonjwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako