• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa waraka juu ya mafunzo ya ufundi stadi mkoani Xinjiang

    (GMT+08:00) 2019-08-16 10:31:42

    China imetoa waraka juu ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi katika mkoa wa Xinjiang.

    Waraka huo uliotolewa leo na Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China, umesema ugaidi na msimamo mkali ni adui wa binadamu, na vita dhidi ya ugaidi na msimamo mkali ni jukumu la pamoja la jamii ya kimataifa. Waraka huo pia umesema, ni kazi muhimu kwa kila serikali inayowajibika, kuchukua hatua za kanuni za msingi kuondoa ugaidi na msimamo mkali ambavyo vinatishia maisha ya watu na usalama, kulinda hadhi ya watu na thamani yao, kulinda haki yao ya kuishi, afya na maendeleo, na kuhakikisha wanafurahia mazingira ya amani na masikilizano ya kijamii.

    Waraka huo umeongeza kuwa ili kushughulikia dalili na vyanzo, na kuchukua hatua za kuzuia na za kupambana kwa pamoja, mkoa wa Xinjian umeanzisha vituo vya elimu na mafunzo ya ufundi stadi kuendana na sheria ili kuzuia kuanza na kuenea kwa ugaidi na msimamo mkali wa kidini, kuzuia kwa ufanisi matukio ya mara kwa mara ya kigaidi na kulinda haki ya kuishi, afya, na maendeleo ya watu wa makabila yote, na kwamba mafanikio yamepatikana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako