• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Polisi wa Hong Kong wawakamata watu watano kwa kuitusi bendera ya taifa

  (GMT+08:00) 2019-08-16 16:50:51

  Polisi wa Hong Kong wamesema leo wamekamatwa watu watano kwa tuhuma za kuitusi bendera ya taifa.

  Watu hao watano, wakiwemo wanaume wanne na mwanamke mmoja wenye umri kati ya miaka 20 na 22, walikamatwa Agosti 14 na 15 katika maeneo ya Mong Kok, Ma On Shan, Sham Shui Po, Ngau Tu Kok na Wong Tai Sin. Polisi pia wamekamata kompyuta, simu na nguo kwenye makazi yao kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

  Agosti 3 na 5, waandamanaji wenye msimamo mkali walishusha bendera kwenye mlingoti wake huko Tsim Sha Tsui, Peninsula ya Kowloon na baadaye kuzitupa baharini. Kwa mujibu wa sheria wa ya Bendera ya taifa na Nembo ya taifa ya Mkoa wa Utawala Maalumu wa Hong Kong, mtu anayeharibu bendera ya taifa au nembo ya taifa hadharani na kuichoma kwa makusudi, kuichana, kuichora, kuichafua au kuikanyaga anakuwa amefanya makosa. Na kama akihukumiwa, atatozwa faini ya ngazi ya 5 na kufungwa jela kwa miaka mitatu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako