• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Bei ya bidhaa ya China haitapanda kwa kiasi kikubwa katika kipindi kijacho

  (GMT+08:00) 2019-08-16 17:00:09

  Msemaji wa Kamati ya Maendeleo na Mageuzi ya China Bibi Meng Wei amesema, tangu mwanzo wa mwaka huu, bei ya bidhaa inadumishwa katika kiwango mwafaka, na katika kipindi kijacho bei hii haitapanda kwa kiasi kikubwa.

  Takwimu mpya zimeonesha kuwa, mwezi Julai mwaka huu, kiwango cha bei ya bidhaa za matumizi nchini China CPI imepanda kwa asilimia 0.4 kuliko mwezi Juni, ikiwa ni ongezeko la asilimia 2.8 kuliko mwaka jana wakati kama huu. Msemaji wa Kamati ya Maendeleo na Mageuzi ya China Bibi Meng Wei anasema:

  "Katika miezi kadhaa iliyopita, ongezeko la CPI limezidi la mwaka jana wakati kama huu, na kufikia asilimia 2.8 katika mwezi Julai. Uchambuzi umeonesha kuwa, hili ni ongezeko la kimuundo, ambalo limeonekana zaidi katika bei ya chakula. Na ikiwa sekta hii itaondolewa, kiwango cha ongezeko la CPI kinaonesha mwelekeo wa utulivu."

  Bibi Meng pia ameeleza kuwa, katika kipindi kijacho, bei ya bidhaa nchini China haitapanda kwa kiasi kikubwa, kwa sababu kutokana na upande wa utoaji wa bidhaa, kiwango cha jumla cha utoaji wa mazao ya viwanda na kilimo, pamoja na utoaji wa huduma ni cha kutosha. Kutokana na upande wa mahitaji, matumizi ya wakazi yanaongezeka kwa utulivu, hivyo mwelekeo wa kudumisha kiwango cha jumla cha bei ya bidhaa kwa utulivu una msingi thabiti.

  Mkutano wa Ofisi ya mambo ya kisiasa ya Kamati ya Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China umesema, inapaswa kuhakikisha utulivu wa kimsingi wa soko la utoaji wa bidhaa na bei zake. Kutokana na hayo, Bibi Meng Wei amesema, idara husika za Kamati ya Maendeleo na Mageuzi ya China zimechukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa fidia, mikopo na ardhi ili kutuliza bei ya bidhaa. Baadhi ya hatua hizo zimepata ufanisi, na katika siku za baadaye, idara hiyo itaendelea kusimamia mabadiliko ya bei ya bidhaa muhimu za maisha ya watu, na kuchukua hatua kwa wakati na za lazima ili kuhakikisha bei inadumishwa katika kiwango mwafaka.

  Bibi Meng anasema: "Inapaswa kushughulikia vizuri kadiri iwezekanavyo kazi ya kutuliza utoaji wa nafasi za ajira, ili kuweka msingi thabiti kwa kuongeza uwezo wa matumizi ya wakazi. Kutangaza na kutekeleza "Mpango wa kuhimiza mapato ya wakazi mijini na vijijini mwaka 2019-2020", kuhimiza mageuzi ya sekta muhimu ya mambo ya kilimo na vijiji na mfumo wa kusajili wakazi, ili kuongeza mapato ya wakazi na kuimarisha uwezo wao wa matumizi."

  Mkutano huo pia umeweka mipango kuhusu kuzidi kupanua matumizi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako