• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gazeti la Marekani laonya tena kuhusu hatari ya udidimiaji wa uchumi wa Marekani

    (GMT+08:00) 2019-08-16 17:11:40

    Gazeti la Marekani WallStreet Journal limetoa makala ikionya tena kuwa sera ya ushuru ya serikali ya Marekani na hali isiyo na uhakika inayotokana na sera hiyo vitapunguza ongezeko la uchumi wa Marekani au hata kuufanya uchumi huo kudidimia.

    Hii ni mara ya pili kwa gazeti hilo kutoa onyo kama hilo. Wiki iliyopita gazeti hilo lilitoa makala inayoitwa "Udidimiaji wa Navarro" ikimkosoa mkurugenzi wa kamati ya biashara ya taifa ya Ikulu ya Marekani na kuonya kuwa mashambulizi ya kibiashara yasiyo na utaratibu yanaweza kusababisha kupungua kwa ukuaji wa uchumi wa Marekani.

    Gazeti hilo jana lilitoa makala nyingine inayoitwa "Udidimiaji wa Navarro II" huku ikilaani hatari inayotokana na sera ya kuongeza ushuru. Makala hiyo imesema, ingawa sera hiyo haitasababisha udidimiaji wa uchumi mara moja, lakini hali isiyo na uhakika inayotokana na sera hiyo itapunguza biashara za dunia na uchocheaji wa uchumi unaotokana na sera za kupunguza ushuru na kulegeza udhibiti kwa uwekezaji wa mitaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako