Aliyasema hayo wakati akizungumza katika hafla ya kumuaga Nassir Salum Mabrouk ambaye atashiriki tamasha la safari ndefu duniani kwa kutumia usafiri wa boti katika kutembea dunia nzima kupitia baharini.
Alimtaka mshiriki huyo ambaye ni pekee kwa nchi za Afrika Mashariki kuitangaza Zanzibar kiutalii kupitia mashindano hayo.
Kombo alisema iko haja ya kukuza utalii wa bahari ili watalii wanaofika Zanzibar watumie usafiri wa baharini.
Mashindano hayo ya tamasha la safari ndefu duniani, hutumia boti ambayo haitumii mashine na badala yake itakua inategemea upepo na watazunguka mabara sita.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |