• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda yachunguza akaunti 13 za mashirika yasiyo ya kiserikali

    (GMT+08:00) 2019-08-16 18:58:58

    Serikali ya Uganda imeanza kuchunguza kaunti 13 za mashirika yasiyokuwa na serikali nchini humo. Zoezi hilo la kitaifa lilianza rasmi jana na tayari benki ya Equity imeandikiwa barua ya kutaka itoe taarifa ya mashirika 10 yasiyo ya kiserikali. Mamlaka ya kuchunguza uhalifu wa fedha imesema baadhi ya mashirika yanayochunguzwa ni pamoja na shirika la Action Aid Uganda, Citizen Coalition for Democracy, Alliance for Campaign finance Monitoring na Anti-Corruptio Coalition Uganda miongoni mwa mengine. Shirika la Democratic Governance Facility ambalo linafadhiliwa na mashirika saba ya maendeleo ya kimataifa pia ni miongoni mwa mashirika ambayo yanachunguzwa. Kwa mujibu wa idara ya takwimu nchini Uganda kuna mashirika yasiyo ya kiserikali 14,207 lakini ni mashirika 3,810 pekee ambayo yamesajiliwa rasmi nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako