• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wawekezaji wa Tanzania na Afrika Kusini watakiwa kukumbatia fursa za uwekezaji katika nchi zote mbili

    (GMT+08:00) 2019-08-16 18:59:50

    Marais wa Tanzania na Afrika Kusini wamewataka wafanya biashara na wawekezaji wa pande zote mbili kunufaika na fursa za uwekezaji hususan katika sekta ya viwanda katika nchi zote mbili.

    Marais hao wamesema hayo katika hafla iliyojumuisha pia watendaji wanaosimamia taasisi za uwekezaji, sekta binafsi pamoja na wafanyabiashara wa nchi hizo.

    Mkutano huo wa kunadi vivutio vya uwekezaji ulikuwa sehemu ya Mkutano wa baraza la wafanyabiashara la Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (Sadc), likikutanisha Tanzania na Afrika Kusini.

    Magufuli alisema kwa kuwa Afrika Kusini imefanikiwa katika ujenzi wa viwanda kama vya magari, kuna nafasi kwa nchi hiyo kujenga Tanzania.

    Ramaphosa amesema hivi sasa Afrika Kusini inaendelea kiviwanda na ni muhimu kushirikisha sekta binafsi nchini Tanzania ili kufikia malengo yanayohitajika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako