Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje wa Russia Bi. Maria Zakharova amesema kuwa operesheni yoyote ndani ya Syria inatakiwa kupata ruhusa ya serikali ya Syria, kwa sababu inahusu mamlaka ya nchi hiyo.
Akiongea na wanahabari Bi. Zakharova amesema kama nchi yenye mamlaka, Syria inatakiwa kudhibiti hali yake ya ndani na kutoa maamuzi husika, na kwamba Russia haikubali sababu yoyote ya kuigawa Syria, na msimamo huo hautabadilika kamwe, haswa operesheni ya Uturuki nchini humo, na kutumai kuwa Uturuki itatekeleza makubaliano yaliyofikiwa mwezi Septemba mwaka jana mjini Sochi kati ya nchi hizo mbili.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |