• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNHCR lasema watu wanaokimbia wanamgambo kwenye eneo la Ebola nchini DRC wanahitaji msaada

    (GMT+08:00) 2019-08-17 18:23:03

    Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Matifa UNHCR, limesema watu wanaowakimbia wanamgambo kwenye eneo la mlipuko wa Ebola huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanaongezeka na wanahitaji msaada wa kibinadamu.

    Msemaji wa UNHCR Babar Balochi, amesema katika wiki tatu za mwezi Juni pekee, zaidi ya watu laki 1.45 wametafuta usalama na msaada kwenye maeneo yaliyotengwa ya Ituri, huku watu laki 1.25 wakikadiriwa kukimbilia maeneo jirani.

    Kwa mujibu wa Shirka la Afya Duniani WHO, watu wanaokimbia nchini DRC pia wanazuia juhudi za kukabiliana na mlipuko wa virusi vya Ebola, ambavyo vimeathiri sehemu za mashariki mwa Ituri na jimbo la Kivu Kaskazini nchini DRC.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako