• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Tanzania awa mwenyekiti mpya wa SADC, akitoa wito wa kuwa kanda ya kiviwanda

    (GMT+08:00) 2019-08-18 17:24:53

    Rais wa Tanzania John Magufuli jana aliteuliwa kuwa mwenyekiti mpya wa zamu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC.

    Kiongozi huyo wa Tanzania amechukua uenyekiti wa SADC kutoka kwa rais wa Namibia Hage Geingob. Akihutubia baada ya kuchukua uenyekiti kwenye mkutano wa kilele wa 39 wa wakuu wa nchi na serikali huko jijini Dar es Salaam, amesema haikubaliki kwamba kanda iliyojaaliwa maliasili nyingi halafu inabaki kuwa masikini.

    "Nchi zetu sio masikini. Ni tajiri sana. Tuna kila aina ya rasilimali tunayohitaji ili nchi kuwa tajiri. Mbali na idadi kubwa ya watu wapatao milioni mia tatu na ishirini saba, nchi za SADC ni nyumbani kwa idadi kubwa ya wanyama pori na spishi za mimea. Ambazo ni muhimu sana. Na bila kusahau mifugo na viumbe wa baharini. Hali kadhalika nchi zetu zina madini na mafuta na gesi asilia"

    Magufuli pia ameiomba jumuiya ya kimataifa kuondoa vikwazo ilivyowekewa Zimbabwe, akisema nchi imekuwa na mabadiliko ambayo kwa sasa yanaifanya kuwa nchi ya kidemokrasia.

    "Kama tunavyofahamu kuwa Zimbabwe imewekewa vikwazo kwa muda mrefu. Vikwazo hivi haviathiri watu wa Zimbabwe na serikali yake tu, bali vinaathiri kanda nzima. Hivyo ningependa kutumia fursa hii kuiomba jumuiya ya kimataifa kuondoa vikwazo iliyoiwekea zimbabwe. Kwani juu ya yote hivi sasa Zimbabwe imefungua ukurasa mpya na iko tayari kushirikiana na ulimwengu mzima"

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako