• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wajumbe wa pande tatu wajadiliana suala la Yemen huko Tehran

    (GMT+08:00) 2019-08-18 17:24:56

    Wajumbe wa pande tatu za serikali za nchi nne za Ulaya, kundi la Houthi la Yemen na serikali ya Iran jana walifanya mazungumzo kuhusu suala la Yemen huko Tehran. Wakati huohuo maafisa wa serikali ya Yemen walidokeza kuwa, jeshi la tume ya mpito ya kusini limeanza kuondoka kwenye maeneo kadhaa mjini Aden na kuweka mazingira mazuri kwa mazungumzo hayo.

    Wajumbe wa pande hizo tatu walieleza misimamo yao na kubadilishana maoni juu ya hali ya sasa ya vita nchini Yemen, hali ya siasa na hali ya haki za binadamu. Pande hizo tatu zilikubaliana kuwa, Yemen inapaswa kusimamisha vita na kutatua mgogoro kwa njia ya kisiasa, na kufuata makubaliano yaliyofikiwa kati ya serikali ya Yemen na kundi la Houthi la Yemen mwezi Disemba mwaka 2018 huko Stockholm.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako