• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Russia yasema inapenda kuzungumza na Marekani juu ya suala la makombora ya masafa ya kati ya kinyuklia

    (GMT+08:00) 2019-08-19 09:10:31

    Waziri wa ulinzi wa Russia Bw. Sergei Shoigu amesema ingawa Marekani imejitoa rasmi kwenye Mkataba wa makombora ya kinyuklia ya masafa ya kati INF, Russia itaendelea kufanya mazungumzo na nchi hiyo juu ya makombora hayo.

    Shoigu amesema Russia iko tayari kwa mazungumzo na Marekani, na haitachukua hatua kabla ya mifumo ya makombora ya masafa ya kati ya kinyuklia kuwekwa huko Ulaya, Asia na Pasifiki. Wizara ya ulinzi ya Russia imependekeza mara nyingi kufanya mazungumzo na Marekani juu ya kurejesha mkataba wa INF kuanzia mwezi Februari mwaka huu, lakini haikupata majibu kutoka Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako