• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SADC yapongeza Zanzibar kwa maendeleo ya utalii

    (GMT+08:00) 2019-08-19 19:02:39

    Wajumbe wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umeisifu Zanzibar baada ya kuridhishwa na maendeleo ya sekta ya utalii pamoja na juhudi za kulinda historia ya nchi.

    Dhlamina Nkoso kutoka Swaziland, mmoja wa wajumbe hao, amependezwa na juhudi za kuitangaza Zanzibar katika sekta ya utalii duniani na kusema Zanzibar inauzika katika soko la utalii kutokana na historia na majengo ya kale.

    Alisema amepata nafasi ya kutembelea visiwani vingi duniani na kuijumuisha Zanzibar miongoni mwa visiwa vyenye historia na maeneo ya kuvutia katika utalii.

    Baadhi ya maeneo waliyotembelea wageni hao ni kanisa la Mkunazini ambalo lilikuwa soko la watumwa pamoja na mahandaki ya chini kwa chini yaliyoko Hurumzi eneo la Mji Mkongwe.

    Akizungumza na ujumbe huo, Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda wa Zanzibar Hassan Khamis Hafidh, alisema Serikali ya Zanzibar imejipanga katika kulitumia soko la nchi za (SADC) katika biashara za aina mbalimbali kwa wananchi wake wakiwamo wajasiriamali.

    Alisema hivi sasa tayari wafanyabiashara kutoka Zanzibar wanalitumia vizuri soko la dagaa lililoko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

    Alisema mikakati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa sasa ni kuimarisha soko la bidhaa za viungo kama vile pilipili manga, pipilipi hoho na uzile.

    Miongoni mwa mikakati inayochukuliwa kwa sasa ni kuitangaza Zanzibar katika ramani ya dunia ya utalii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako