• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • PAC yailaumu NCPB kwa kutoelezea jinsi Sh440m zilitumika katika ununuzi wa magunia

    (GMT+08:00) 2019-08-19 19:03:12

    Wabunge wa Kenya wameilaumu Bodi ya Kitaifa ya Nafaka na Mazao (NCPB) kwa kutowajibikia matumizi ya Sh440.1 milioni zilizotengwa kwa ajili ya ununuzi wa magunia ya kuhifadhi mahindi katika mwaka wa kifedha uliokamilika Juni 30, 2017.

    Kamati ya Bunge kuhusu Uhasibu wa Pesa za Umma (PAC) ilielezwa kwamba bodi hiyo ilitumia jumla ya Sh841.6 milioni kwa ununuzi wa magunia lakini ni Sh401.5 milioni pekee ambazo matumizi yake yaliwajibikiwa.

    Katibu wa Wizara ya Kilimo Profesa Hamadi Boga aliyefika mbele ya Kamati hiyo alikabiliwa na wakati mgumu kueleza ni kwa nini wizara yake haikutoa maelezo kuhusu jinsi ambavyo Sh440,092,022 zilizosalia zilitumika.

    Hii ni baada ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Edward Ouko, kwenye ripoti yake ya ukaguzi wa matumizi ya fedha katika NCPB mwaka huo, kusema bodi hiyo haikutoa stakabadhi kuhusu namna kiasi hicho cha fedha kilitumika.

    Lakini Profesa Boga aliwaambia wanachama wa kamati ya PAC kwamba hitalafu hiyo ilitokana na changamoto inayokabiliwa NCPB katika mfumo wa sasa wa "usimamizi na uhifadhi wa nafaka".

    Profesa Boga pia alikabiliwa na wakati mgumu kuelezea tofauti katika bei ya magunia ya mahindi kwa waliopewa zabuni ya kuwasilisha magunia hayo.

    Ilibainika kuwa baadhi ya wafanyabiashara waliuza magunia hayo kwa Sh38.28 kila moja huku wengine wakiwasilisha bidhaa hiyo kwa NCPB kwa bei ya Sh28.08 kwa kila gunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako