• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOMAFCO kuanzisha kiwanda cha kubangua Korosho

    (GMT+08:00) 2019-08-19 19:05:16

    Shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha kuwezesha vijana kielimu na kiuchumi (SOMAFCO) linatarajia kuanzisha kiwanda cha kubangua korosho mkoani Morogoro nchini Tanzania.

    SOMAFCO itaanzisha kiwanda hicho ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono mahitaji ya Tanzania katika uwekezaji wa viwanda vya kuungua zao hilo.

    Kauli hiyo imetolewa jana Alhamisi Agosti 15,2019 kupitia Mkutano wa Baraza la Wafanyabiashara wa Nchi 16 za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

    Mkuu wa SOMAFCO, TIholo Mohlathe amesema Tanzania na Afrika Kusini zimekuwa zikishirikiana kwa kipindi kirefu tangu kupigania uhuru hivyo kwa sasa kituo hicho kitachochea ukuaji wa shughuli za uzalishaji wa zao hilo.

    Katika kipindi cha kupigania ukombozi kusini mwa Afrika, SOMAFCO kilikuwa ni chuo cha Wapigania Uhuru wa Afrika kusini cha Solomoni Mahalangu, mkoani Morogoro.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako