• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Uganda yalalamikia vikwazo vya mipkani

    (GMT+08:00) 2019-08-20 19:59:37

    Uganda imeomba kuondolewa kwa vikwazo vinavyowekewa mizigo katika maeneo ya mipakani ili kurahisisha biashara.

    Waziri wa biashara nchini humo Amelia Kyambadde amesema pia ufisadi kwenye vituo hivyo unachangia hasara ya asilimia 20 kwa wafanyabiashara wa Uganda.

    Kyambadde anataja vikwazo vingine kuwa ni pamoja na sera dhaifu, ushuru na vikwazo visivyo vya ushuru.

    Balozi wa Kenya nchini Uganda Kiema Kilonzo amesema zaidi ya asilimia 82 ya shehena za Uganda hupitia katika bandari ya Mombasa nchini Kenya na inatarajiiwa kuongezeka kufuatia kuanza kwa oparesheni za reli mpya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako