• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania- Benki ya maendeleo ya Afrika yaipa Tanzania bil. 400

    (GMT+08:00) 2019-08-20 19:59:53

    Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imeipatia serikali ya Tanzania Dola za Marekani milioni 180 (Sh. bilioni 414.07) kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa barabara ya njia nne, kuzunguka Jiji la Dodoma yenye urefu wa kilometa 110.2 kwa kiwango cha lami.

    Halfa ya utiaji saini wa mkopo huo ilifanyika jana jijini Dar es Salaam, huku ilielezwa kuwa kukamilika kwa mradi huo kutaiwezesha Tanzania kufikia azma yake ya kuwa kitovu cha biashara na usafirishaji katika ukanda wa mashariki na kusini mwa Afrika.

    Akizungumza katika hafla hiyo, Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James, alisema kusainiwa kwa mkataba huo kutaongeza kiasi cha fedha ambazo zimetengwa na AfDB kwa ajili ya miradi ya ujenzi wa barabara nchini kutoka Dola za Marekani milioni 858.16 hadi Dola bilioni 1,038 (Sh. trilioni 2.39).

    Doto James, alisema serikali imetenga Sh. bilioni 284 kwa ajili ya kuzipati halmashauri zitakazoandika andiko la mradi utakaoingizia fedha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako