• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Korea yatafuta nafasi ya kuwekeza kwenye Zanzibar

    (GMT+08:00) 2019-08-20 20:00:12

    Kampuni ya Kimataifa ya uzalishaji wa umeme unaotumia gesi ya nchini Korea Kusini (FCCPP) imesema Zanzibar ina rasilimali nyingi za uwekezaji ikiwamo mazingira bora ya hali ya hewa.

    Imesema mazingira hayo yanawapa moyo wa kuanzisha mradi wao unaokuwa ndani ya bahari masafa ya mita 100, umbali wa ardhi unaoambatana na mita 10 chini ya bahari.

    Mwakilishi wa kampuni hiyo, Profesa Injoon Suh, alisema hayo wakati timu yake ikitangaza nia yao ya kutaka kuwekeza mradi wao mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, Vuga Mjini Zanzibar.

    Prof. Injoon Suh, alisema, umeme unaozalishwa na kampuni hiyo unaweza kabisa kutumia gesi asilia inayozalishwa nchini Tanzania kwa kuongezea na ile inayopatikana kutoka Mashariki ya Kati.

    Alisema kiwango cha umeme utakaozalishwa na kampuni hiyo yenye uzoefu na utaalamu wa masuala ya nishati ya gesi unafikia megawatts 215 kiwango ambacho ni kikubwa kwa Zanzibar kinachoweza kutosheleza mahitaji yote ya huduma hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako