• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania na Kenya zatarajia kukua kwa sekta ya utalii

    (GMT+08:00) 2019-08-20 20:01:53

    Tanzania na Kenya zinatarajia ukuaji chanya wa sekta yake ya utalii na hoteli katika kipindi cha miaka 5 ijayo, licha ya hali isiofahamika ya kiuchumi, kupungua kwa uwekezaji wa kigeni na tishio la ugaidi.

    Ripoti ya shirika la Price Water Coopers inaonyesha kuwa mikutano, na maendeleo ya miundo mbinu kwenye nchi hizo itasaidia kukua kwa sekta ya utalii.

    Aidha hoteli za kimataifa kama vile Radisson, Marriot, Best Western, Sheraton, Ramada, Hilton na Mövenpick zimefungua matawi Afrika Mashairki kukidhi idadi ya wageni inayotarajiwa kuongezeka.

    Ripoti ya Hotels Outlook Mwaka 2019–2023 inaonyesha kuwa ukuaji wa miradi ya hiteli nchini Tanzania na Kenya ndio wa juu zaidi barani Afrika ukiwa na ongezeko la asilimia 8 kwa mwaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako