• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Miradi ya nishati inayochelewa kutekelezwa inawagharimu wakenya mabilioni ya pesa,asema Waziri wa nishati,Charles Keter

    (GMT+08:00) 2019-08-22 19:17:58

    Miradi ya nishati iliyocheleweshwa utekelezaji wake inawakosesha wakenya umeme wa bei nafuu.

    Haya ni kwa mujibu wa Waziri wa Nishati nchini Kenya,Charles Keter,ambaye alisema ucheleweshwaji una gharama zake ambazo hatimaye zinaathiri bei ya umeme ambao uanasambaziwa wateja.

    Alisema miradi mingi ya nguvu za umeme imechelewa kutokana na kesi mahakamani.

    Aliongeza kuwa miradi mingi ya umeme mara nyingi imekumbwa na changamoto kutoka kwa jamii,na kusababisha kucheleweshwa kwa miradi hiyo na kuongezeka kwa gharama.

    Miongoni mwa miradi iliyoathirika iko chini ya Kampuni ya usambazaji umeme ya Ketraco ambayo imekuwa ikitekeleza miradi ya 400kV, 220kV na 132kV , ambayo ucheleweshwaji wake umesababisha walipa ushuru kupewa adhabu kubwa.

    Ucheleweshaji pia umekubwa katika mradi wa 400Kv wenye umbali wa kilomita 428 kutoka Loyiangalani kwenda Suswa uliojengwa kwa ajili ya kuhamisha umeme mradi wa nishati ya upepo uliozinduliwa hivi karibuni wa megawati 310 ulioko Turkana,ambapo walipa ushuru walitozwa faini ya Sh3.8 bilioni.

    Mmoja wa mkandarasi wa Ketraco alitoza Sh108 million kwa mwezi,ambapo alisema vifaa vyake vimekaa bure kwa miezi 21.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako