• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Biashara Afrika Mashariki (EABC) lapata ufadhili wa $3.2m kwa ajili ya uwezeshaji biashara

    (GMT+08:00) 2019-08-22 19:18:35

    Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC) jumanne lilitia saini mkataba wa ufadhili wa US$ 3.2 milioni na shirika la TradeMark East Africa (TMEA) kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa mpango wa miaka mitatu wa kurahisisha na usawazishaji wa taratibu za biashara katika ukanda huo.

    Ushirikiano huu utasaidia juhudi za EABC za kuboresha uratibu,na azimio la kuondolewa kwa vikwazo visivyokuwa vya ushuru katika ushoroba wa Afrika mashariki;kuoanisha na kupitisha viwango vya Afrika Mashariki;kuboresha upitishaji na uoanishaji wa sera za forodha na kodi za ndani na uwezeshaji wa biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki.

    Afisa Mkuu Mtendaji wa EABC,Peter Mathuki,alisema wataratibu na kufanya utafiti wa ithibati kuhusu mazungumzo kati ya sekta za umma na binafsi katika kupunguza vikwazo vya kufanya biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako