• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jamii mbalimbali za Hong Kong zataka kuzuia mabavu na vurugu kwa kufuata sheria na kurejesha jamii katika hali ya kawaida

    (GMT+08:00) 2019-08-23 19:52:13

    Mkutano wa pamoja wa vyama vya kibiashara vya sekta mbalimbali vya Hong Kong, Shirika la Henry Fok, na wadau wa uchukuzi wa ardhini wa Hong Kong wametoa taarifa kwenye magazeti kadhaa wakilaani vikali kitendo chochote cha kukiuka sheria na kutoa wito kwa wakazi kuunga mkono serikali ya Hong Kong na polisi kuzuia mabavu na vurugu na kuirejesha jamii katika hali ya kawaida.

    Mkutano wa pamoja wa vyama vya kibiashara vya sekta mbalimbali vya Hong Kong umetoa taarifa ikisema utaunga mkono polisi kutekeleza sheria kwa makini, kuhimiza kurejesha utaratibu wa jamii na kulaani vikali tukio la kimabavu lililotokea katika uwanja wa ndege lililoathiri sifa ya Hong Kong katika jumuiya ya kimataifa.

    Kwa upande wa Shirika la Henry Fok, limesema vurugu zabarabarani zinazoendelea kupamba moto zimeathiri vibaya utawala wa kisheria na utulivu wa jamii, ambazo pia zimetishia vibaya usalama wa maisha na mali za wakazi wa Hong Kong na kuathiri vibaya taswira ya Hong Kong. Hivi sasa, Hong Kong inatakiwa kuzuia mabavu na vurugu, kulinda utawala wa kisheria, kuwaadhibu wahalifu, kurejesha utaratibu na kushikilia moyo wa mwanzo na majukumu ya sera ya "Nchi Moja, Mifumo Mwili" na kukataa kabisa vitendo vya kimabavu.

    Nao wadau wa uchukuzi wa ardhini wa Hong Kong wamesema, maandamano na vitendo vya kimabavu vimeziba barabara na kusababisha mabasi ya abiria na malori ya mizigo kukosa njia ya kwenda, mapato ya madereva yanapungua kwa kiasi kikubwa na maisha yao yameathiriwa vibaya. Wamewataka waandamanaji kukaa na kufikiria, njia pekee ya kuona siku za mbele zenye mustakabali mzuri ni kuirejesha Hong Kong katika utulivu haraka iwezekanavyo.

    Habari nyingine zinasema, ombi la kuongeza muda wa amri ya kuweka vizuizi kwa muda lililotolewa na idara ya usimamizi wa uwanja wa ndege wa Hong Kong kwa mahakama kuu ya Hong Kong limeidhinishwa na jaji, amri ambayo itadumu mpaka mahakama itoe amri nyingine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako