• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yapongezwa kwa kuboresha sekta ya elimu

    (GMT+08:00) 2019-08-23 20:15:40

    Benki ya Dunia (WB) imepongeza Tanzania kwa kutoa kipaumbele kwa sekta ya elimu nchini humo kwa jinsi inavyohakikisha watoto wenye umri wa kwenda shule wanapata nafasi hiyo.

    Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia ukanda wa nchi za Afrika Bi Anne Kabagambe alisema hayo alipofanya ziara katika shule ya Sekondari Kibasila akiwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa, Joyce Ndalichako.

    Kabagambe alitembelea shule hiyo kwa sababu Benki ya Dunia inaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika juhudi zinazofanywa kwenye sekta ya elimu ikitambua elimu ni ndio chimbuko la maendeleo katika mchi yoyote.

    Kwa upande wake, Waziri Ndalichako alisema Benki ya Dunia imekuwa ikishirikiana na Serikali katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo mradi wa elimu unaojulikana kama Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R) ambapo WB imetoa dola za kimarekani milioni 202 katika mradi huo ulioanza kutekelezwa mwaka 2014 na unategemewa kumalizika mwaka 2021.

    Alisema kupitia mradi huo takribani shilingi bilioni 141 zimetumika kwa ajili ya kukarabati shule kongwe 62, kujenga vyumba vya madarasa 2,876, matundu ya vyoo 6,558, nyumba za walimu 59, mabwalo 76, majengo ya utawala 16, mabweni 533 kwa ajili ya kuwaepusha watoto wa kike na changamoto za mbalimbali, pamoja na kujenga mifumo ya maji safi kwenye baadhi ya shule ambazo hazikuwa na vyanzo vya maji.

    Waziri Ndalichako alisema kwa upande wa Shule ya Sekondari Kibasila Sh900 milioni zimetengwa kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2019/2020 kwa ajili ya ukarabati na tayari wataalamu wameanza kufanya tathmini ya majengo ya shule hiyo ambayo ukarabati wake utaanza wakati wowote kuanzia sasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako