• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mwenyekiti wa Baraza la Ulaya atoa wito wa kusimamisha vita ya biashara

  (GMT+08:00) 2019-08-25 18:22:18

  Mwenyekiti wa Baraza la Ulaya Bw. Donald Tusk amesema vita ya biashara lazima isimamishwe mara moja, na kwamba dunia nzima itaathiriwa vibaya kama Marekani ikitumia njia ya kuongeza ushuru kama silaha kutokana na sababu za siasa.

  Akizungumza na wanahabari kabla ya kufunguliwa kwa mkutano wa viongozi wa kundi la nchi saba zilizoendelea kiviwanda duniani G7, Bw. Tusk amesema makubaliano ya biashara na mageuzi ya Shirika la Biashara Duniani WTO ni ufumbuzi mzuri kuliko vita ya biashara, kwani vita ya biashara itadhoofisha uchumi, lakini makubaliano ya biashara yataendeleza uchumi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako