• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maonesho ya vitabu ya kimataifa ya Beijing yahimiza biashara ya hakimiliki

    (GMT+08:00) 2019-08-26 07:54:14

    Maonesho ya 26 ya kimataifa ya vitabu ya Beijing yaliyomalizika jana Jumapili yameshuhudia jumla ya biashara 5,996 za hakimiliki za ndani na nje, ikiwa ni ongezeko la asilimia 5.6 kuliko mwaka jana.

    Maonesho hayo ya siku tano yalivutia wachapishaji zaidi ya 2,600 kutoka nchi na sehemu 95 duniani.

    Katika kuadhimisha miaka 70 ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, maonesho maalumu ya vitabu na majarida yanayoonesha maendeleo ya China na sekta ya uchapishaji katika miongo saba iliyopita, pia yalifanyika kwenye maonesho hayo.

    Aidha, shughuli zaidi ya 1,180 za kiutamaduni ziliandaliwa na kuwavutia watazamaji laki 3.2.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako