• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uwezekano wa Uingereza kufikia makubaliano na Umoja wa Ulaya kuhusu Brexit waongezeka

  (GMT+08:00) 2019-08-26 08:24:59

  Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema, uwezekano wa Uingereza kufikia makubaliano na Umoja wa Ulaya kuhusu kujitoa kwenye Umoja huo umeongezeka.

  Bw. Johnson amefanya mazungumzo kwa mara ya kwanza na mwenyekiti wa Baraza la Ulaya Bw. Donald Tusk na kusema, anatarajia Uingereza itajitoa kwenye Umoja huo chini ya makubaliano nao, na ameliita suala la mpaka la Ireland kuwa ni kinyume cha demokrasia. Pia amesema hatazuia bunge la nchi hiyo kuendelea kujadiliana kuhusu suala la Brexit.

  Habari zinasema, wanasiasa wanaounga mkono Uingereza kujitoa kwenye Umoja huo na wanaopinga Uingereza kujitoa bila ya makubaliano, wanaendelea na majadiliano ili kujiandaa vizuri kwa ajili ya mkutano wa bunge utakaoanza Septemba 3.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako