• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mavutano kati ya Rwanda na majirani wake imesababisha kupungua kwa kasi kwa biashara ya mipakani

    (GMT+08:00) 2019-08-26 19:43:37
    Mavutano kati ya Rwanda na majirani wake imesababisha kupungua kwa kasi kwa biashara ya mipakani, na takwimu za hivi karibuni za benki kuu zinaonyesha kushuka kwa mauzo ya nje kwa asilimia 8.1, wakati uagizaji ulipungua kwa asilimia 40 katika nusu ya kwanza ya mwaka huu ikilinganishwa na 2018.

    Mauzo ya nje yasiyo rasmi iliandikisha asilimia 10 ya jumla ya mauzo ya nje ya nchi wakati uagizaji usio rasmi uliandikisha asilimia 0.5.

    Mvutano ya mapema kati ya Rwanda na Burundi pia iliathiri biashara isiyo rasmi na iliyo rasmi ya mipakani kati ya nchi hizo mbili, haswa baada ya Bujumbura kuzuia wafanyabiashara wake kuuza mboga kwenda Rwanda.

    Uuzaji wa jumla usio rasmi wa Rwanda mnamo 2018 ulifikia dola milioni 125.3. Mauzo ya nje kwa nchi zingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambayo ni asilimia 22.3 ya mauzo yake yote, hata hivyo, iliongezeka kwa asilimia 141.0 kwa thamani, kuvutia dola milioni 128.9 katika nusu ya kwanza ya 2019.

    Uagizaji kutoka mkoa huo hata hivyo umepungua kwa asilimia 7.8, kwa sababu ya kuongezeka kwa biashara za ndani ambazo zilibidi kujinadi na kujaza pengo la watumiaji wa bidhaa kutoka Uganda na Burundi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako