• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya yauza nje mapipa laki  2 ya mafuta

  (GMT+08:00) 2019-08-27 08:24:44

  Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametangaza kuwa nchi hiyo imesafirisha kwa mara ya kwanza mapipa laki 2 ya mafuta kutoka bandari ya Mombasa hadi Uingereza, hivyo kuifanya Kenya kuwa nchi ya kwanza ya Afrika Mashariki kuuza mafuta nje.

  Rais Kenyatta amesema, mafuta hayo yenye kiwango cha chini cha sulphur yaliyozalishwa katika kaunti ya Turkana, kaskazini magharibi mwa nchi hiyo, yana thamani ya dola za kimarekani milioni 12 ambayo ni ya juu zaidi kuliko bei iliyokadiriwa.

  Maofisa wa nishati wamesema, mauzo hayo yanalenga kutathmini mapokezi ya soko ya kimataifa kwa mafuta hayo kabla ya uzalishaji wa kibiashara unaotarajiwa kuanza mwaka 2023.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako