• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Afrika Kusini yapongeza mafunzo yanayotolewa na polisi wa China

  (GMT+08:00) 2019-08-27 08:44:56

  Msemaji wa idara ya polisi ya Johannesburg, Afrika Kusini Bw. Wayne Minnaar amesema mafunzo ya wiki mbili yaliyotolewa na polisi wa China kwa wenzao wa Johannesburg yatasaidia kupunguza uhalifu mjini humo. Ameongeza kuwa cha muhimu katika mafunzo hayo ni kuwafundisha maofisa hao ufundi kwa vitendo, ambapo wanaweza kufanya mazoezi ya kujilinda bila ya silaha na hatua za kuwadhibiti wahalifu wakati wanapowakamata. Pia mafunzo hayo ni pamoja na kanuni za kiufundi kuhusu hatua za ghafla wanazoweza kuchukua wanapoingia katika nyumba au jengo kukabiliana na wahalifu wenye silaha.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako